Jarida la Mapishi

Supu ya nyanya

Supu ya nyanya | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 25
  • Walaji
    6

Supu ya nyanya, ni supu tamu yenye krimu, inayopendwa sana kunywewa na watu wakati wa kipindi cha kiangazi. Supu hii inakuwa tamu zaidi endapo itapikwa kwa kutumia nyanya nzuri na zilizo iva vizuri. Fuata hatua zifuatazo, ili kujifunza jinsi ya kupika supu hii ya nyanya.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za binzari nyembamba kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step2

    Chukua kinu. Weka ndani ya hicho kinu mbegu za binzari nyembamba ulizo zikaanga, kisha twanga hadi utakapo ona mbegu hizo zimesagika vizuri.

    Step3

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu maji pamoja na tangawizi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena.

    Step4

    Weka kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, karoti pamoja na viazi mviringo, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena jingine.

    Step5

    Weka nyanya kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona nyanya hizo zimesagika vizuri na kuwa laini.

    Step6

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka mchanganyiko wa vitunguu maji ulio usaga kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step7

    Weka mchanganyiko wa karoti ulio usaga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step8

    Ongeza moto na uweke moto mkubwa. Weka nyanya ulizo zisaga, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3.

    Step9

    Weka maji, chumvi, pamoja na sukari halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na uache ichemke.

    Step10

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 15, kisha epua uweke pembeni ili ipoe.

    Step11

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, supu uliyo ipika, kisha saga hadi utakapo ona supu hiyo imesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa supu hiyo kwenye mashine ya kusaga na urudishe kwenye sufuria. Weka sufuria hilo kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha ichemke.

    Step12

    Chukua kikombe chenye maziwa. Weka unga wa mahindi ndani ya hicho kikombe chenye maziwa halafu koroga vizuri, kisha mimina kwenye sufuria lenye supu.

    Step13

    Weka binzari nyembamba pamoja na kungumanga halafu koroga vizuri, kisha epua na umimine kwenye kontena.

    Step14

    Mimina mtindi ndani ya hilo kontena lenye supu, kisha koroga vizuri, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.