-
Maandalizi-
-
KupikaSaa 1
-
Walaji4
Kuku wa kuoka, ni pishi rahisi kupika ambalo nadhani mtu yoyote anayependa kupika anapaswa kulifahamu. Unachohitaji katika kupika pishi hili, ni viungo, chumvi pamoja na mafuta ya kupikia. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika kuku huyu wa kuoka.
Ingredients
Directions
Chukua nyama ya kuku na uondoe ngozi yake yote.
Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, mtindi, mafuta ya kupikia, giligilani, vitunguu swaumu, tangawizi, pilipili manga, iliki, binzari nyembamba, mbegu za uwatu, pamoja na chumvi, kisha changanya hadi utakapo ona viungo vyote vimechanganyika vizuri.
Chukua nyama ya kuku na uiweke kwenye hilo kontena kubwa lenye viungo, kisha changanya vizuri, hadi utakapo ona upande wote wa nje na upande wa ndani ya tumbo la huyo kuku umechanganyika vyema na viungo. Funika vizuri kontena kwa kutumia mfuniko au plastic wrap, kisha weka kwenye friji kwa muda wa kati ya saa 2 hadi saa 24.
Washa jiko la kuoka na uweke joto la nyuzi 204° C, kisha acha jiko lipate moto. Chukua sinia la kuoka. Weka kuku juu ya hilo sinia, huku miguu ikiwa inatizama upande wa juu. Mimina juu ya kuku mchanganyiko wa viungo uliobaki kwenye kontena, halafu mpake vizuri kuku wote hivyo viungo ulivyomimina.
Nyunyizia juu ya huyo kuku, mdalasini, karafuu na majani ya minti, kisha funika nyama ya kuku kwa kutumia aluminium foil, halafu weka kwenye jiko la kuoka na uoke kwa muda wa dakika 40 au hadi utakapo oja upande wa juu wa kuku umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Baada ya dakika 40, fungua jiko la kuoka na utoe sinia la kuoka lenye kuku. Fungua aluminum foil, halafu geuza kuku juu chini, kisha funika tena kwa aluminium foil. Rudisha tena hiyo nyama ya kuku kwenye jiko la kuoka, kisha punguza moto na uweke joto la nyuzi 190° C. Eendelea kuoka kuku huyo kwa muda wa kati ya dakika 20 mpaka 30.
Kuku akisha iva, ondoa kutoka kwenye jiko la kuoka na umuweke pembeni kwa muda wa dakika 5, kabla ya kula.
Recipe Reviews