-
MaandaliziDakika 15
-
KupikaDakika 45
-
Walaji8
Keki ya strawberry, ni keki rahisi sana kupika. Keki hii yawezekana ikawa ndio keki tamu kuliko keki zote ulizowahi kupika au kula katika maisha yako. Ulaiji wa keki hii ya strawberry, ni njia moja ya kula na kufaidi faida za kiafya za matunda ya steawberry. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya strawberry.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi, pamoja na sukari, kisha changanya vizuri.
Weka mayai, mtindi na vanilla extract, halafu endelea kuchanganya.
Weka unga wa ngano, baking powder, pamoja na matunda ya strawberry, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40 mpaka 45, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.
Leave a Review