-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 10
-
Walaji4
Mishikaki ya nyama ya ng'ombe, ni mishikaki mitamu inayopikwa kwa kutumia nyama ya ng'ombe iliyokatwa vipande vipande vipande na kuchanganywa pamoja na viungo, kisha kuchomwa kwenye jiko la kuchomea nyama. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mishikaki hii ya nyama ya ng'ombe.
Ingredients
Directions
Chukua kontena dogo. Weka ndani ya hilo kontena, nyama ya ng'ombe, tangawizi, vitunguu swaumu, garam masala, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya nyama ya ng'ombe vimeenea vyema viungo.
Funika kontena hilo vizuri, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 2.
Baada ya saa 2, ondoa kontena hilo kwenye friji na uliweke pembeni.
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, mtindi, limao, nazi, pamoja na iliki, kisha changanya vizuri. Mimina mchanganyiko huu kwenye kontena lenye mchanganyiko wa nyama ya ng'ombe, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya nyama ya ng'ombe vimeenea vyema mchanganyiko huu.
Funika kontena hilo vizuri, kisha liweke tena kwenye friji kwa muda wa saa 4.
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka vijiti vya mishikaki ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.
Baada ya dakika 30, mwaga maji yote yaliyomo kwenye kontena na kubakiwa na vijiti peke yake.
Chukua vijiti vya mishikaki, kisha chomeka vipande vya nyama ya ng'ombe kwenye hivyo vijiti.
Washa jiko la kuchomea nyama, kisha acha jiko lipate moto. Weka mishikaki juu ya jiko la kuchomea nyama, kisha choma mishikaki hiyo huku ukigeuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona pande zote za mishikaki hiyo zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Ondoa mishikaki hiyo kwenye jiko la kuchomea nyama na uiweke kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review