-
MaandaliziDakika 20
-
KupikaDakika 40
-
Walaji10
Mkate wa blackberry na mahindi, ni mkate mtamu ambao wafaa kula kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi au kama kitafunio cha kawaida wakati wa mchana. Utamu wa mkate huu, unatokana hasa na matunda halisi ya blackberry pamoja na unga wa mahindi, vilivyo changanywa katika mkate huu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mkate huu wa blackberry na mahindi.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, unga wa mahindi ya njano, unga wa ngano, chumvi, pamoja na baking powder, kisha changanya vizuri.
Weka mayai, mtindi, mafuta ya kupikia, maziwa na matunda ya blackberry, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutumia ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka mkate (loaf pan), na uweke ndani ya hilo sufuria karatasi ya kuokea (baking paper). Mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganyia, ndani ya hilo sufuria la kuoka mkate.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Mkate ukishaiva, uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria la kuoka mkate. Mkate ukishapoa, unaweza kuutoa ndani ya sufuria la kuoka mkate, na kuukata kwa ajili ya kula.
Leave a Review