Jarida la Mapishi

Mkate wa mtindi

Mkate wa mtindi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 20
  • Kupika
    Dakika 40
  • Walaji
    8

Mkate wa mtindi, ni mkate rahisi sana kupika ambao unapikwa kwa kutumia mahitaji machache tu. Tofauti na mikate mingine, mapishi ya mkate huu hayahitaji kuweka hamira. Unaweza kula mkate huu pamoja na mchuzi au supu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mkate huu wa mtindi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, unga wa ngano, baking powder, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Weka mayai, mtindi, maziwa ya lozi, vanilla extract na mafuta ya kupikia, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step3

    Chukua sufuria la kuoka mkate (loaf pan), na uweke ndani ya hilo sufuria karatasi ya kuokea (baking paper). Mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganyia, ndani ya hilo sufuria la kuoka mkate.

    Step4

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step5

    Mkate ukishaiva, uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria la kuoka mkate. Mkate ukishapoa, unaweza kuutoa ndani ya sufuria la kuoka mkate, na kuukata kwa ajili ya kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.