-
MaandaliziDakika 35
-
KupikaDakika 40
-
Walaji10
Keki ya berry na limao, ni keki tamu laini inayofaa kuliwa katika kipindi cha masika. Keki hii hupikwa kwa kutumia matunda halisi ya berry yalioiva, limao iliyokamuliwa pamoja na maganda ya limao yaliyo kunwa. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya berry na limao.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi, pamoja na sukari, kisha changanya vizuri.
Weka mayai, maganda ya limao yaliyo kunwa, limao iliyo kamuliwa na mtindi, halafu endelea kuchanganya.
Weka unga wa ngano, baking powder, chumvi, pamoja na matunda ya berry, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 8, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 35 mpaka 40, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.
Leave a Review