-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 25
-
Walaji4
Saladi ya viazi mviringo, ni saladi tamu na rahisi kutengeneza, ambayo hutengezwa kwa kutumia viazi mviringo, vitunguu vya kijani, mtindi pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya viazi mviringo.
Ingredients
Directions
Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za binzari nyembamba kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.
Chukua kinu. Weka ndani ya hicho kinu mbegu za binzari nyembamba ulizo zikaanga, kisha twanga hadi utakapo ona mbegu hizo zimesagika vizuri.
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona vimeiva.
Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.
Menya maganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka ndani ya hilo kontena, mtindi, ¼ kijiko cha chai cha chumvi, pilipili manga, pamoja na vitunguu vya kijani, kisha changanya vizuri.
Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka viazi mviringo ulivyo vichemsha kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3.
Weka tangawizi, majani ya giligilani, pamoja na ½ kijiko cha chai cha chumvi, halafu endelea kukaanga huku ukivigeuza viazi mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 zaidi, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia, kisha epua na uweke pembeni kwenye kontena.
Chukua kontena lenye mchanganyiko wa mtindi na umimine kwenye kontena lenye mchanganyiko wa viazi mviringo.
Nyunyizia binzari nyembamba uliyo itwanga, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review