-
MaandaliziDakika 30
-
KupikaDakika 45
-
Walaji10
Keki ya maboga, ni keki inayopikwa kwa kutumia boga lililo sagwa pamoja na viungo. Keki hii yafaa kula kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi, au kama kitindamlo, au kama kitafunio cha kawaida. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya maboga.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, unga wa ngano, baking powder, chumvi, baking soda, pamoja na mdalasini, kisha changanya vizuri.
Chukua bakuli nyingine ndogo. Weka ndani ya hiyo bakuli, mafuta ya kupikia pamoja na sukari, kisha changanya kwa muda wa dakika 2. Weka mayai, na uendelee kuchanganya. Weka maboga, vanilla extract na maziwa, kisha changanya vizuri.
Chukua mchanganyiko wa bakuli ndogo ya pili, na umimine kwenye mchanganyiko wa bakuli la kwanza, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 45, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.
Leave a Review