-
MaandaliziDakika 35
-
KupikaDakika 40
-
Walaji10
Keki ya aramoni na chocolate, ni keki tamu na rahisi kupika yenye ladha ya mchanganyiko wa njugu za aramoni pamoja na chocolate. Keki hii yafaa kula kama kitindamlo baada ya mlo wowote ule au kwenye sherehe. Fuata hatia zifuatszo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya aramoni na chocolate.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, mafuta ya kupikia, siagi na dark chocolate chips, kisha weka bakuli hilo kwenye sufuria lenye maji ya moto, halafu acha siagi pamoja na dark chocolate chips viyeyuke.
Ukiona vimeyeyuka, ondoa bakuli kwenye sufuria lenye maji ya moto na uliweke pembeni. Weka sukari na aramoni, kisha changanya vizuri.
Weka cocoa powder, unga wa ngano, lozi, chunvi, pamoja na baking powder, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 35 mpaka 40, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.
Leave a Review