-
MaandaliziDakika 20
-
KupikaDakika 40
-
Walaji10
Mkate wa maboga na machungwa, ni mkate ambao asili yake ni kutoka nchini Ukrainia. Mkate huu hupikwa kwa kutumia boga lilio sagwa, machungwa yaliyo kamuliwa, maganda ya machungwa yaliyo kunwa pamoja na viungo. Mkate huu wafaa kula katika sikukuu za krismasi au sherehe ya aina yoyote ile. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mkate huu wa maboga.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, boga, maganda ya chungwa, chungwa lililo kamuliwa, mayai, pamoja na vanilla extract, kisha changanya vizuri.
Weka unga wa ngano, chumvi, baking powder, mdalasini, tangawizi na kungumanga, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka mkate (loaf pan), na uweke ndani ya hilo sufuria karatasi ya kuokea (baking paper). Mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganyia, ndani ya hilo sufuria la kuoka mkate.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Mkate ukishaiva, uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria la kuoka mkate. Mkate ukishapoa, unaweza kuutoa ndani ya sufuria la kuoka mkate, na kuukata kwa ajili ya kula.
Leave a Review