Jarida la Mapishi

Maboga yenye komamanga

Maboga yenye komamanga | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Saa 1 Dk. 15
  • Walaji
    4

Maboga yenye komamanga, ni chakula ambacho hupikwa kwa kutumia maboga, viungo, pamoja na mbegu za kokamanga zilizo kaushwa na kusagwa. Mbegu za komamanga ambazo huwekwa katika chakula hiki, husaidia kuongeza ladha na kukifanya chakula hiki kiwe kitamu zaidi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika maboga haya yenye komamanga.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mbegu za uwatu, pamoja na mbegu za giligilani, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.

    Step2

    Weka maboga, binzari ya manjano pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona maboga yamebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step3

    Punguza moto na uweke moto mdogo. Mimina maji, halafu funika sufuria na uache ichemke huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona maboga yameiva, kisha epua na uweke pembeni.

    Step4

    Weka sukari, mbegu za komamanga, pamoja na majani ya minti halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na uache itulie kwa muda wa dakika 30 mpaka 40.

    Step5

    Rudisha sufuria kwenye jiko halafu acha maboga yapate moto, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.