-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 1
-
Walaji4
Saladi ya matango na karanga, ni saladi tamu ambayo hutengenezwa kwa kutumia matango, karanga zilizo kaangwa, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Saladi hii yafaa kula katika msimu wa kiangazi, pamoja na chakula chochote ukipendacho. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya matango na karanga.
Ingredients
Directions
Chukua kontena. Weka ndani ya hilo kontena, matango, karanga, majani ya giligilani, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri.
Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali, curry powder, pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa sekunde kadhaa. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye kontena lenye saladi, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.
Leave a Review