Jarida la Mapishi

Mchuzi wa tanipu

Mchuzi wa tanipu | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 35
  • Walaji
    4

Mchuzi wa tanipu, ni mchuzi wenye ladha nzuri ambao hupikwa kwa kutumia tanipu, majani ya tanipu, vitunguu maji, nyanya, pamoja na viungo. Mchuzi huu wa tanipu, wafaa kula pamoja na chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa tanipu.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mbegu za kisibiti, pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

    Step2

    Weka tangawizi, majani ya tanipu, pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step3

    Weka nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.

    Step4

    Weka mbegu za giligilani, binzari ya manjano, chumvi, pamoja na tanipu, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.

    Step5

    Mimina maji halafu koroga vizuri. Ongeza moto na uweke moto mkubwa, kisha funika sufuria na uache ichemke.

    Step6

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona tanipu zimeiva na mchuzi umekuwa mzito.

    Step7

    Weka majani ya giligilani pamoja na garam masala, halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.