-
Maandalizi-
-
Kupika-
-
Walaji1
Achari ya giligilani na limao, ni achari tamu ambayo hutengenezwa na kutumia majani ya giligilani, majani ya minti, pilipili hoho, limao, vitunguu vya kijani, pamoja na viungo. Achari hii yafaa kutumika kwenye sandwiches, sambusa, au kwenye kitafunio chochote kile ukipendacho. Pia unaweza kutumia achari hii kwenye nyama yoyote ile ya kuchoma. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza achari hii ya giligilani na limao.
Ingredients
Directions
Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za binzari nyembamba kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.
Chukua kinu. Weka ndani ya hicho kinu mbegu za binzari nyembamba ulizo zikaanga, kisha twanga hadi utakapo ona mbegu hizo zimesagika vizuri.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, tangawizi, pilipili hoho, pamoja na vitunguu vya kijani, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri.
Weka majani ya giligilani pamoja na majani ya minti, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema.
Weka limao, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Weka Chaat Masala, sukari, pamoja na chumvi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena.
Weka binzari nyembamba uliyo ikaanga ndani ya hilo kontena, kisha changanya vizuri.
Weka achari hiyo kwenye chombo safi chenye mfuniko, kisha hifadhi kwenye friji.
Leave a Review