Jarida la Mapishi

Samaki wa kuchoma

Samaki wa kuchoma | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 10
  • Walaji
    4

Samaki wa kuchoma, ni kitoweo kitamu na chenye ladha ya kipekee ambacho huchomwa kwa kuchanganywa na nazi, limao, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Kitoweo hiki cha samaki wa kuchoma, chafaa kula pamoja na wali au tambi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika samaki wa kuchoma.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, mafuta ya kupikia, mbegu za kisibiti, chumvi, tangawizi, vitunguu swaumu, tui la nazi, binzari nyembamba, pamoja na limao, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Weka vipande vya minofu ya samaki, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya samaki vimeenea vyema viungo. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 4 mpaka saa 12.

    Step3

    Washa jiko la kuchomea nyama, kisha acha lipate moto.

    Step4

    Chukua wavu wa kuchomea nyama. Paka mafuta vizuri wavu huo, kisha uweke kwenye jiko.

    Step5

    Weka vipande vya minofu ya samaki juu ya wavu, halafu choma kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona vimeiva. Ondoa vipande hivyo vya minofu ya samaki kwenye jiko la kuchomea na uviweke pembeni kwenye chombo safi. Kumbuka kugeuza minofu hiyo mara 1 au 2 wakati unachoma.

    Step6

    Nyunyizia Chaat Masala, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.