Jarida la Mapishi

Saladi ya vitunguu na limao

Saladi ya vitunguu na limao | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    -
  • Walaji
    4

Saladi ya vitunguu na limao, ni saladi tamu na maarufu, ambayo hutengenezwa kwa kutumia vitunguu maji, limao, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Saladi hii yafaa kula pamoja na chapati, pilau, biriani, au pamoja na wali wa aina yoyote ile. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya vitunguu na limao.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena. Weka ndani ya hilo kontena, vitunguu maji pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri. Funika vizuri kontena hilo, kisha acha kwa muda wa saa 2.

    Step2

    Chukua chujio, kisha chuja maji yaliyomo kwenye kontena na kubakiwa na vitunguu maji peke yake.

    Step3

    Chukua kontena jingine. Weka ndani ya hilo kontena, vitunguu maji, majani ya giligilani, limao, pamoja na tangawizi, kisha changanya vizuri. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 2. Baada ya saa 2, ondoa saladi kwenye friji, kisha iweke pembeni, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.