Jarida la Mapishi

Achari ya minti

Achari ya minti | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    -
  • Walaji
    1

Achari ya minti, ni achari yenye ladha nzuri ambayo hutengenezwa kwa kutumia majani ya minti, majani ya giligilani, kitunguu maji, limao, pamoja na viungo. Achari hii yafaa kula pamoja na kitafunio chochote kile ukipendacho, kama vile sambusa, sandwich, au chapati, fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika achari hii ya minti.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu maji, limao, pamoja na vijiko 2 vya chakula vya maji, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri.

    Step2

    Weka majani ya minti pamoja na majani ya giligilani, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema.

    Step3

    Weka vijiko 2 vya chakula vya maji vilivyobaki, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step4

    Weka mbegu za komamanga, pilipili manga, sukari, pamoja na chumvi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni.

    Step5

    Weka achari hiyo kwenye chombo safi chenye mfuniko, kisha hifadhi kwenye friji.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.