Jarida la Mapishi

Samaki wa kukaanga

Samaki wa kukaanga | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 15
  • Walaji
    4

Samaki wa kukaanga, ni kitoweo kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kuchanganya samaki, limao, ukwaju, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Kitoweo hiki cha samaki wa kukaanga, chafaa kula pamoja na wali mweupe, wali wa binzari nyembamba, wali wa nazi, au wali wa ukwaju. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika kitoweo hiki cha samaki wa kukaanga.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, vipande vya minofu ya samaki, vitunguu swaumu, pilipili manga, garam masala, mbegu za kisibiti, Tamarind Paste, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya samaki vimeenea vyema viungo. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 1 mpaka saa 4.

    Step2

    Chukua kikaango kikubwa chenye vijiko 1½ vya chakula vya mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto mkubwa, kisha acha mafuta yapate moto kwa muda wa dakika 2. Weka vipande vya minofu ya samaki kwenye hicho kikaango, kisha kaanga kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona upande wa chini wa vipande hivyo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step3

    Nyunyizia mafuta ya kupikia yaliyobaki juu ya vipande hivyo vya samaki.

    Step4

    Geuza upande wa pili wa vipande hivyo vya samaki, halafu kaanga kwa muda wa dakika 4, au hadi utakapo ona na upande huo wa pili, umebadilika rangi na kuwa rangi ya kahawia, kisha epua na uweke pembeni kwenye chombo safi.

    Step5

    Nyunyizia limao juu ya vipande hivyo vya samaki, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.