-
MaandaliziDakika 30
-
KupikaDakika 15
-
Walaji4
Wali wa binzari ya manjano (Wali wa manjano), ni chakula rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kutumia mchele pamoja na viungo mbalimbali kama vile binzari ya manjano. Wali huu wafaa kula pamoja na mboga, kuku wa kuchoma, au mishikaki. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika wali huu wa binzari ya manjano.
Ingredients
Directions
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.
Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, mchele, maji uliyotumia kurowekea mchele, binzari ya manjano, chumvi, pilipili manga, pamoja na iliki, halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.
Zima jiko, kisha acha wali utulie kwa muda wa dakika 5, ukiwa bado juu ya jiko. Baada ya dakika 5, pakua wali kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review