Jarida la Mapishi

Wali wa kijani

Wali wa kijani | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 30
  • Kupika
    Dakika 20
  • Walaji
    4

Wali wa kijani, ni chakula kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kutumia mchele, spinachi, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Wali huu wafaa kula pamoja na saladi yoyote ya mboga. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika wali huu wa kijani.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.

    Step2

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, spinachi pamoja na majani ya uwatu, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step3

    Chukua sufuria kubwa na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha sufuria lipate moto. Weka mchanganyiko ulio usaga kwenye hilo sufuria, kisha kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 5.

    Step4

    Weka mchele, maji uliyotumia kurowekea mchele, chumvi, pamoja na pilipili manga, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

    Step5

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

    Step6

    Zima jiko, kisha acha pilau itulie kwa muda wa dakika 5, ikiwa bado juu ya jiko.

    Step7

    Nyunyizia garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.