Jarida la Mapishi

Achari ya giligilani

Achari ya giligilani | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    -
  • Walaji
    1

Achari ya giligilani, ni achari nzuri na rahisi kutengeneza, ambayo hutengenezwa kwa kutumia majani ya giligilani, choroko, ukwaju, pamoja na viungo. Achari hii yafaa kutumia kwenye nyama choma, sambusa au sandwich. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza achari hii ya giligilani.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali pamoja na choroko, halafu kaanga huku ukitikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona choroko zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step2

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga mchanganyiko ulio ukaanga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri.

    Step3

    Weka Tamarind Paste pamoja na majani ya giligilani, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.

    Step4

    Weka chumvi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.

    Step5

    Weka achari hiyo kwenye chombo safi chenye mfuniko, kisha hifadhi kwenye friji.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.