-
MaandaliziDakika 30
-
KupikaDakika 25
-
Walaji4
Pilau ya giligilani na njegere, ni chakula kitamu na chenye afya, ambacho hupikwa kwa kutumia mchele, majani ya giligilani, njegere, vitunguu maji, pamoja na viungo vingine vya aina mbalimbali. Chakula hiki chafaa kula pamoja na mchuzi wa kuku, mchuzi wa nyama ya ng’ombe, mchuzi wa samaki, au mchuzi wa maharage. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya giligilani na njegere.
Ingredients
Directions
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, madalasini, iliki, pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona vitunguu vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Ongeza moto na uweke moto mkubwa. Weka vitunguu swaumu, njegere, majani ya giligilani, garam masala, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.
Weka mchele pamoja na maji uliyotumia kurowekea mchele, halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.
Zima jiko, kisha acha pilau itulie kwa muda wa dakika 5, ikiwa bado juu ya jiko. Baada ya dakika 5, pakua pilau kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review