-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 35
-
Walaji4
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vimeiva.
Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.
Menya maganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.
Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, mbegu za komamanga pamoja na mbegu za giligilani, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Weka viazi mviringo pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7.
Weka majani ya giligilani pamoja binzari nyembamba, halafu endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5 zaidi, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kula.
Leave a Review