Jarida la Mapishi

Biringanya za kuponda zenye njegere

Biringanya za kuponda zenye njegere | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 35
  • Walaji
    4

Biringanya za kuponda zenye njegere, ni mboga ambayo hupikwa kwa kutunia biringanya zilizopondwa, vitunguu maji, nyanya, njegere, cream, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mboga hii yafaa kula pamoja na wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biringanya hizi za kuponda zenye njegere.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena. Weka biringanya ndani ya hilo kontena, halafu funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye jiko la microwave na upike katika moto mkubwa kwa muda wa dakika 5 mpaka 6, au hadi utakapo ona biringanga zimeiva. Ondoa kontena hilo kwenye jiko la microwave na uliweke pembeni ili biringanya zipoe, kisha ziponde vizuri.

    Step2

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

    Step3

    Weka vitunguu swaumu, mbegu za giligilani, binzari nyembamba, garam masala, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step4

    Weka nyanya pamoja na majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.

    Step5

    Weka biringanya ulizo ziponda pamoja na njegere, kisha koroga vizuri.

    Step6

    Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15.

    Step7

    Weka cream halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 1. Epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.