-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 30
-
Walaji4
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, iliki, mdalasini, binzari nyembamba, nyama ya kusaga, vitunguu maji, vitunguu swaumu, tangawizi, majani ya mvuje, mbegu za giligilani, garam masala, mbegu za uwatu, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona nyama imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka spinachi pamoja na majani ya giligilani, kisha endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3, au hadi hadi utakapo ona spinachi imenyauka.
Weka tui la nazi na ukoroge vizuri, kisha funika sufuria na uache ichemke kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito. Epua na upakue kwenye chombo safi tayari kwa kula.
Leave a Review