-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 20
-
Walaji4
Ingredients
Directions
Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka tangawizi kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka binzari nyembamba pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 5, au hadi utakapo ona vimeiva.
Weka tanipu, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 4.
Punguza moto na uweke moto mdogo. Weka sukari halafu koroga vizuri, kisha funika kikaango na upike mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 5 mpaka 7.
Weka majani ya giligilani, kisha endelea kukaanga mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 zaidi.
Nyunyizia garam masala na ukoroge vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review