Jarida la Mapishi

Wali wa ukwaju

Wali wa ukwaju | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 30
  • Walaji
    4

Wali wa ukwaju, ni chakula ambacho hufaa kula katika sherehe za aina mbalimbali, hasa za kidini. Chakula hiki hupikwa kwa kutumia mchele, karanga, dengu, korosho, ukwaju, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifumze jinsi ya kupika wali huu wa ukwaju.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, mchele, maji, pamoja na chumvi halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

    Step2

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

    Step3

    Zima jiko, kisha acha wali utulie kwa muda wa dakika 5, ukiwa bado juu ya jiko. Baada ya dakika 5, pakua wali kwenye kontena, kisha funika vizuri kontena hilo.

    Step4

    Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za giligilani kwenye hicho kikaango, kisha kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1. Ondoa mbegu hizo kwenye kikaango na uziweke pembeni kwenye kontena, kisha acha zipoe.

    Step5

    Weka mbegu za ufuta kwenye kikaango hicho hicho, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30, kisha epua na uweke pembeni. Ondoa mbegu hizo kwenye kikaango na uziweke kwenye kontena lenye mbegu za giligilani, kisha acha zipoe.

    Step6

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mbegu za giligilani pamoja na mbegu za ufuta ulizo zikaanga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke kwenye kontena lenye wali, kisha changanya vizuri.

    Step7

    Chukua kikaango kingine kidogo chenye kijiko 1 cha chakula cha mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, karanga, korosho, pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara, hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa mchanganyiko huo kwenye kikaango na uweke kwenye kontena lenye mchanganyiko wa wali, kisha changanya vizuri.

    Step8

    Weka kwenye kikaango hicho hicho, kijiko 1 cha chakula cha mafuta ya kupikia yaliyobaki, kisha acha mafuta yapate moto. Weka mbegu za haradali, mbegu za uwatu, dengu, pamoja na binzari ya manjano, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara, hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step9

    Weka Tamarind Paste, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1 mpaka 2. Epua mchanganyiko huo na umimine kwenye kontena lenye mchanganyiko wa wali, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.