-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 45
-
Walaji4
Pilau ya uwatu, ni chakula kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kutumia mchele, viazi mviringo, majani mabichi ya uwatu, pamoja na viungo. Chakula hiki chafaa kula pamoja na kinywaji cha mtindi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya uwatu.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria ndogo. Weka maji kiasi, chumvi kiasi pamoja na kiazi, halafu chemsha kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona kiazi kimeiva, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe. Menya maganda yote ya hicho kiazi, kisha kikate katika vipande vidogo vidogo.
Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka majani ya uwatu kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.
Weka viazi, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha endelea kukaanga mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona majani ya uwatu yamebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Epua mchanganyiko huo na uweke kwenye pilau ya binzari nyembamba.
Nyunyizia garam masala juu ya hiyo pilau, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.
Leave a Review