Jarida la Mapishi

Kuku wa giligilani na apple

Kuku wa giligilani na apple | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 40
  • Walaji
    4

Kuku wa giligilani na apple, ni kitoweo kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia nyama ya kuku, majani ya giligilani, matunda ya apple, vitunguu maji, mtindi, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Kitoweo hiki chafaa kula pamoja ma wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika kitoweo hiki cha kuku wa giligilani na apple.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena. Weka ndani ya hilo kontena, vipande vya nyama ya kuku, tangawizi, vitunguu swaumu, limao, mtindi, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya nyama ya kuku vimeenea vyema viungo. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 4 mpaka saa 24.

    Step2

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mbegu za giligilani, pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step3

    Weka vitunguu maji pamoja na binzari ya manjano, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step4

    Weka mchanganyiko wa kuku ulio uweka kwenye friji, kisha pika mchanganyiko huo huku ukivigeuza vipande vya nyama ya kuku mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7.

    Step5

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, majani ya giligilani pamoja na apple kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke kwenye sufuria lenye mchanganyiko wa kuku.

    Step6

    Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha acha ichemke huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 25, au hadi utakapo ona vipande vya nyama ya kuku vimeiva.

    Step7

    Weka garam masala halafu koroga vizuri, kisha acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5 zaidi. Epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.