-
Maandalizi-
-
Kupika-
-
Walaji2
Lemonade ya raspberry na minti, ni kinywaji rahisi kutengeneza, chenye ladha nzuri na cha kuburudisha, ambacho hutengenezwa kwa kusaga pamoja matunda ya raspberry, limao, apple, majani ya minti pamoja na maji. Kinywaji hiki chafaa sana kunywa katika msimu wa kiangazi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza lemonade hii ya raspberry na minti.
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, malimao, matunda ya apple, matunda ya raspberry, majani ya minti, maji, pamoja na sukari, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Chukua chujio, kisha chuja lemonade hiyo vizuri.
Mimina lemonade kwenye chombo safi, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi, kabla ya kunywa.
Conclusion
Unaweza kuongeza maji zaidi, endapo utaona maji yaliyomo katika lemonade hii ni kidogo.
Leave a Review