Jarida la Mapishi

Kuku wa komamanga

  • Maandalizi
    Saa 2
  • Kupika
    Dakika 30
  • Walaji
    4

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukia kontena. Weka ndani ya hilo kontena, vipande vya nyama ya kuku, viazi mviringo, tomato sauce, tangawizi, vitunguu swaumu, majani ya giligilani, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya nyama ya kuku vimeenea vyema viungo. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 2.

    Step2

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mdalasini pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukiroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona vitunguu vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step3

    Weka mchanganyiko wa kuku, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona mchuzi wote umekauka.

    Step4

    Weka mbegu za komamanga, mbegu za giligilani, pamoja na garam masala, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.

    Step5

    Weka pilipili hoho halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.