-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 45
-
Walaji4
Kuku wa pichi na nyanya, ni chakula kilicho sheheni ladha ya utamu na uchachu, ambacho hupikwa kwa kutumia nyama ya kuku, pichi, limao, vitunguu maji, nyanya, pamoja na viungo. Kitoweo hiki chafaa kula pamoja na wali au mkate, hasa katika msimu wa kiangazi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika kitoweo hiki cha kuku wa pichi na nyanya.
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, tangawizi, vitunguu swaumu, pichi, pamoja na nyanya, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Ongeza moto na uweke moto mkubwa. Weka mbegu za giligilani, binzari nyembamba, garam masala, pilipili manga, chumvi, vipande vya nyama ya kuku, pamoja na mchanganyiko wa pichi ulio usaga, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7.
Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara, hadi utakapo ona vipande vya nyama ya kuku vimeiva na mchuzi umekua mzito.
Weka limao pamoja na majani ya giligilani, halafu pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review