-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 20
-
Walaji4
Mboga ya karoti, njegere na viazi, ni mboga yenye virutubisho vingi na rahisi kupika, ambayo hupikwa kwa kutumia karoti, njegere, viazi mviringo, pamoja na viungo. Mboga hii yafaa kula kama chakula cha mchana au cha jioni, pamoja na wali au mkate. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mboga hii ya karoti, njegere na viazi.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba pamoja na tangawizi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Ongeza moto na uweke moto mkubwa. Weka mbegu za giligilani, binzari ya manjano, chumvi, karoti, viazi mviringo pamoja na njegere halafu funika sufuria, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara, hadi utakapo ona umepata moto.
Punguza moto na uweke moto wa wastani. Mimina maji, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona viazi vimeiva.
Weka majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.
Weka mango powder pamoja na pilipili manga halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review