Jarida la Mapishi

Mboga ya kabichi, spinachi na viazi

Mboga ya kabichi, spinachi na viazi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 30
  • Walaji
    4

Mboga ya kabichi, spinachi na viazi, ni mboga tamu ambayo hupikwa kwa kutumia kabichi, spinachi, viazi mviringo, nyanya, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Unaweza kula mboga hii pamoja na wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mboga hii ya kabichi na choroko.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vimeiva.

    Step2

    Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.

    Step3

    Menya maganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.

    Step4

    Chukua kikaango kikubwa chenye vijiko 2 vya chakula vya mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, binzari nyembamba, mbegu za giligilani, mbegu za uwatu, binzari ya manjano, kabichi, spinachi, majani ya giligilani, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa mchanganyiko huo kwenye kikaango na uweke pembeni kwenye kontena.

    Step5

    Weka kwenye kikaango hicho hicho, viazi mviringo pamoja na kijiko 1 cha chakula cha mafuta ya kupikia kilichobaki, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.

    Step6

    Weka nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, au hadi utakapo ona nyanya zimekuwa laini. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye kontena lenye mchanganyiko wa kabichi.

    Step7

    Nyunyizia Chaat Masala, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.