Jarida la Mapishi

Maboga ya kusaga yenye karoti

Maboga ya kusaga yenye karoti | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 15
  • Walaji
    4

Maboga ya kusaga yenye karoti, ni chakula kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kutumia maboga yaliyo sagwa, karoti, vitunguu maji, pilipili hoho, pamoja na viungo. Chakula hiki chafaa kula pamoja na wali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika maboga ya kusaga yenye karoti.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chuku sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, maboga, maji, binzari ya manjano, mbegu za uwatu, vitunguu maji, pilipili hoho, mbegu za giligilani, tangawizi, mafuta ya kupikia, binzari nyembamba, karoti, pamoja na vitunguu swaumu, halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

    Step2

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona vimeiva.

    Step3

    Weka majani ya giligilani halafu koroga vizuri, kisha epua na uweke pembeni.

    Step4

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mchanganyiko wa maboga ulio uchemsha, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.