-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 30
-
Walaji4
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, tangawizi, vitunguu swaumu, korosho, mbegu za mpopi, pamoja na vijiko 2 vya chakula vya maji, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Weka garam masala, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, viazi mviringo, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona viazi vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka mchanganyiko wa tangawizi ulio usaga kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 8 mpaka 10.
Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga.
Mimina maji halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na uache ichemke kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona viazi vimeiva na mchuzi umekuwa mzito.
Mimina tui la nazi halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 3.
Weka iliki halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review