-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 45
-
Walaji4
Kuku wa minti na giligilani, ni kitoweo kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia nyama ya kuku, vitunguu maji, limao, majani ya minti, majani ya giligilani, pamoja na viungo vingine vya aina mbalimbali. Kitoweo hiki chafaa kula pamoja na wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika kitoweo hiki cha kuku wa minti na giligilani.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka tangawizi pamoja na vitunguu swaumu, kisha koroga vizuri.
Weka vipande vya nyama ya kuku, chumvi, pilipili manga, pamoja binzari ya manjano, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 17 mpaka 18 au hadi utakapo ona vipande vya nyama ya kuku vimekaribia kuiva.
Weka majani ya giligilani, majani ya minti, pamoja na limao, halafu kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 20 zaidi, au hadi utakapo ona vipande vya nyama ya kuku vimeiva, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review