Jarida la Mapishi

Nyama ya kuchoma

  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Saa 1 Dk. 10
  • Walaji
    6

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu swaumu, tangawizi, majani ya rosemary, pamoja na majani ya minti yaliyo katwa katwa, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo unesagika vizuri na kuwa laini.

    Step2

    Weka limao, asali, garam masala, binzari nyembamba, chumvi, pamoja na mafuta ya kupikia, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.

    Step3

    Chukua mapande ya nyama pamoja na kisu chenye ncha kali, kisha chanja kwenye kila upande wa mapande hayo ya nyama.

    Step4

    Chukua kontena kubwa. Weka mapande ya nyama ndani ya hilo kontena, kisha paka mchanganyiko wa viungo ulio usaga kwenye hayo mapande ya nyama, hadi utakapo ona mapande yote ya nyama yameenea vyema viungo. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 12 mpaka saa 48.

    Step5

    Washa jiko la kuchomea nyama, kisha acha jiko lipate moto. Weka mapande ya nyama juu hilo ya jiko, kisha choma kwa muda wa dakika 15 mpaka 20, au hadi utakapo ona upande wa chini wa mapande hayo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step6

    Geuza upande wa pili wa mapande hayo, kisha choma kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona na upande huo wa pili umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step7

    Endelea kuchoma mapande hayo kwa muda wa dakika 20 mpaka 30, au hadi utakapo ona yemeiva. Kumbuka kugeuza mara 2 hadi 3 wakati unachoma.

    Step8

    Chukua sufuria dogo lenye siagi na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha siagi ipate moto. Weka kwenye hilo sufuria majani ya minti ya unga pamoja na pilipili manga halafu koroga vizuri, kisha zima jiko.

    Step9

    Paka mchanganyiko huo kwenye mapande ya nyama, halafu endelea kuchoma kwa muda wa dakika 5 zaidi, kisha ondoa mapande hayo kwenye jiko la kuchomea na uyaweke kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.