-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 10
-
Walaji1
Achari ya apple na tangawizi, ni achari yenye ladha nzuri, ambayo utengenezaji wake unafanana sana na utengenezaji wa achari ya ukwaju. Achari hutengenezwa kwa kutumia matunda ya apple, tangawizi, sukari, apple cider vinegar, pamoja na viungo. Achari hii yafaa kula pamoja na mkate, chapati, au nyama za kuchoma. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza achari hii ya apple na tangawizi.
Ingredients
Directions
Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za pilipili manga kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.
Chukua sufuria ndogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali, tangawizi, matunda ya apple, nyanya, chumvi, pamoja na sukari, halafu kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mchanganyiko huo ulioupika pamoja na pilipili manga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga, kisha uhifadhi kwenye chombo chenye mfuniko na kutumia kidogo kidogo kwenye chakula cha aina yoyote ile.
Leave a Review