Jarida la Mapishi

Achari ya dengu na karanga

Achari ya dengu na karanga | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 5
  • Walaji
    1

Achari ya dengu na karanga, ni achari yenye ladha nzuri iliyo sheheni virutubisho vya protini kwa wingi, ambayo hutengenezwa kwa kutumia dengu, karanga, limao, dengu, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Achari hii yafaa kutumia kwenye chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza achari hii dengu na karanga.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka dengu kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step2

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga dengu pamoja na karanga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena.

    Step3

    Weka kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, majani ya giligilani pamoja na limao, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema.

    Step4

    Weka mchanganyiko wa dengu na karanga ulio usaga, sukari, pamoja na chumvi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.

    Step5

    Weka achari hiyo kwenye chombo safi chenye mfuniko, kisha hifadhi kwenye friji.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.