-
Maandalizi-
-
Kupika-
-
Walaji1
Achari ya karanga na vitunguu swaumu, ni achari ambayo hutengenezwa kwa kutumia karanga pamoja na viungo vya aina mbalimbali kama vile vitunguu swaumu. Achari hii yafaa kula pamoja na vitafunio vya vifungua kinywa kama vile, chapati, mkate au sandwich. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza achari hii ya karanga na vitunguu swaumu.
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka karanga kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri.
Weka nazi, vitunguu swaumu, Tamarind Paste, pamoja na chumvi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena.
Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali, pamoja na majani ya mvuje, kisha koroga vizuri. Epua mchanganyiko huo na umimine kwenye kontena lenye mchanganyiko ulio usaga, kisha changanya vizuri.
Weka achari hiyo kwenye chombo safi chenye mfuniko, kisha hifadhi kwenye friji.
Leave a Review