-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 1
-
Walaji1
Achari ya maembe mabichi, ni achari ya ambayo hutengenezwa kwa kutumia maembe mabichi, chumvi, sukari, vitunguu vya kijani, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Achari hii yafaa kutumika kwenye chakula cha ina yoyote. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza achari hii ya maembe mabichi.
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, maembe, tangawizi, vitunguu vya kijani, majani ya mvuje, pamoja na chumvi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena.
Weka sukari ndani ya hilo kontena, kisha changanya vizuri.
Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali pamoja na mbegu za uwatu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye kontena lenye mchanganyiko wa maembe, kisha changanya vizuri.
Weka achari hiyo kwenye chombo safi chenye mfuniko, kisha hifadhi kwenye friji.
Leave a Review