-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 10
-
Walaji1
Achari ya minti na maembe, ni achari maarufu ambayo hutengenezwa kwa kutumia majani mabichi ya minti, maembe yaliyoiva, pamoja na viungo. Achari hii yafaa kutumika kwenye vitafunio vya aina mbali mbali, kama vile sambusa. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza achari hii ya minti na maembe.
Ingredients
Directions
Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za binzari nyembamba kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.
Chukua kinu. Weka ndani ya hicho kinu mbegu za binzari nyembamba ulizo zikaanga, kisha twanga hadi utakapo ona mbegu hizo zimesagika vizuri.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, tangawizi, majani ya minti, pamoja na ½ kikombe cha maji, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria dark brown sugar pamoja na vikombe 3 vya maji, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto wa wastani huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 4, au hadi utakapo ona imeyeyuka.
Weka mchanganyiko wa minti ulio usaga, maembe, Chaat Masala, tangawizi ya unga, binzari nyembamba, chumvi, pamoja na black salt, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha acha iendelee kuchemka huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.
Epua mchangayiko huo na uweke pembeni ili upoe, kisha hifadhi achari hiyo kwenye chombo chenye mfuniko na kutumia kidogo kidogo kwenye chakula cha aina yoyote ile.
Leave a Review