Jarida la Mapishi

Achari ya minti, nazi na ukwaju

  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 5
  • Walaji
    1

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za binzari nyembamba kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step2

    Chukua kinu. Weka ndani ya hicho kinu mbegu za binzari nyembamba ulizo zikaanga, kisha twanga hadi utakapo ona mbegu hizo zimesagika vizuri.

    Step3

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, nazi, tangawizi, pamoja na vitunguu swaumu, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema.

    Step4

    Weka majani ya giligilani, majani ya minti, Tamarind Paste, pamoja na chumvi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena.

    Step5

    Weka binzari nyembamba uliyo ikaanga ndani ya hilo kontena, kisha changanya vizuri.

    Step6

    Weka achari hiyo kwenye chombo safi chenye mfuniko, kisha hifadhi kwenye friji.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.