Jarida la Mapishi

Achari ya nyanya

Achari ya nyanya | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 25
  • Walaji
    1

Achari ya nyanya, ni achari tamu ambayo hutengenezwa kwa kutumia tomato sauce, vitunguu maji, choroko, dengu, ukwaju, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Achari hii yafaa kutumia kwenye kifungua wakati wa asubuhi. Pia waweza kutumia achari hii kwenye wali au kitafunio chichote kile ukipendacho. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza achari hii ya nyanya.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mbegu za giligilani, mbegu za binzari nyembamba, choroko, dengu, pamoja na mbegu za pilipili manga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri.

    Step2

    Chukua sufuria dogo lenye mafuya ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali, majani ya mvuje, vitunguu swaumu, pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa sekunde kadhaa.

    Step3

    Weka mchanganyiko ulio usaga pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.

    Step4

    Punguza moto na uweke moto mdogo. Weka tomato sauce pamoja na Tamarind Paste, halafu funika sufuria, kisha acha ichemke huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona achari imekuwa nzito. Epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step5

    Weka achari hiyo kwenye chombo safi chenye mfuniko, kisha hifadhi kwenye friji.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.