Jarida la Mapishi

Achari ya ufuta na karanga

Achari ya ufuta na karanga | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 5
  • Walaji
    1

Achari ya ufuta na karanga, ni achari yenye ladha nzuri, ambayo hutengenezwa kwa kutumia mbegu za ufuta, karanga, ukwaju, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Achari hii yafaa kutumia kwenye vitafunio vya vifungua kinywa wakati wa asubuhi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza achari hii ya ufuta na karanga.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za ufuta mweupe kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, kisha epua na uweke pembeni.

    Step2

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mbegu za ufuta mweupe ulizo zikaanga, karanga, vitunguu swaumu, Tamarind Paste, majani ya giligilani, chumvi, pamoja na maji ya moto, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step3

    Weka achari hiyo kwenye chombo safi chenye mfuniko, kisha hifadhi kwenye friji.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.