-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 30
-
Walaji4
Ingredients
Directions
Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka bamia kwenye hicho kikaango, kisha kaanga bila kutumia mafuta huku ukizigeuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona bamia zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Epua na uweke pembeni kwenye kontena.
Weka mafuta ya kupikia kwenye kikaango hicho hicho. Weka vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona vimeiva.
Weka bamia ulizo zikaanga mwanzoni, kisha kaanga huku ukizigeuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3.
Weka mbegu za giligilani, binzari nyembamba, mango powder, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.
Weka majani ya giligilani, kisha endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 zaidi.
Nyunyizia garam masala na ukoroge vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review