-
MaandaliziDakika 30
-
KupikaSaa 1 Dk. 40
-
Walaji4
Biriani ya kuku, ni chakula kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia mchele, nyama ya kuku, maziwa, mtindi, kaukau za vitunguu maji, nyanya, zafarani, pamoja na viungo vingine vingi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biriani hii ya kuku.
Bofya HAPA ili kujifunza jinsi ya kupika kaukau za vitunguu maji, ambazo utazitumia katika kupika biriani hii ya kuku.
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu swaumu, tangawizi, nyanya, pamoja na kikombe 1 cha majani ya giligilani, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena kubwa.
Weka kwenye hilo kontena, mtindi, garam masala, pamoja na kijiko 1 cha chai cha chumvi, kisha koroga vizuri.
Weka nyama ya kuku, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya nyama ya kuku vimeenea vyema viungo. Funika kontena hilo vizuri, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 8 mpaka saa 24.
Chukua kikombe chenye maziwa, kisha roweka zafarani ndani ya hicho kikombe chenye maziwa kwa muda wa dakika 30.
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, mchele, maji uliyotumia kurowekea mchele, pamoja na ½ kijiko cha chai cha chumvi, halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu acha iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona maji kwenye sufuria yamekaribia kukauka na wali haujaiva, kisha epua na uweke pembeni. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.
Mwaga maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na wali peke yake.
Chukua sufuria jingine kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, iliki, mdalasini, majani ya mbei, binzari nyembamba, pamoja na mchanganyiko wa kuku ulio uweka kwenye friji halafu koroga vizuri, kisha zima jiko.
Weka kaukau za vitunguu maji, ½ kikombe cha majani ya giligilani, pamoja na majani ya minti juu ya huo mchanganyiko wa kuku, kisha sambaza vizuri.
Weka wali juu ya hivyo viungo, kisha sambaza vizuri.
Nyunyizia maziwa yenye zafarani juu ya huo wali.
Funika vizuri sufuria hilo kwa kutumia aluminium foil, kisha weka mfuniko juu ya hilo aluminium foil.
Washa jiko na uweke moto mkubwa, kisha pika biriani hiyo kwa muda wa dakika 10.
Punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha endelea kupika biriani hiyo kwa muda wa dakika 15.
Punguza moto tena na uweke moto mdogo, kisha endelea kupika biriani hiyo kwa muda wa saa 1, au hadi utakapo ona biriani imeiva.
Zima jiko, kisha changanya biriani hiyo vizuri, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review