-
MaandaliziDakika 30
-
KupikaSaa 1 Dk. 50
-
Walaji4
Biriani ya mbavu, ni chakula kitamu ambacho chafaa kuliwa hasa wakati wa sherehe. Biriani hii hupikwa kwa kutumia, pilau ya binzari nyembamba, viungo, mtindi, pamoja na mbavu za mbuzi au mbavu za kondoo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biriani hii ya mbavu.
Bofya HAPA ili kujifunza jinsi ya kupika pilau ya binzari nyembamba, ambayo utaitumia katika kupika biriani hii ya mbavu.
Ingredients
Directions
Chukua kikombe chenye maziwa, kisha roweka zafarani ndani ya hicho kikombe chenye maziwa kwa muda wa dakika 30.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, nyama za mbavu, tangawizi, vitunguu swaumu, garam masala, pamoja na chumvi, kisha kaanga upande huo wa kwanza wa nyama za mbavu kwa muda wa dakika 2 mpaka 3, au hadi utakapo ona upande huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Geuza upande wa pili wa nyama hizo za mbavu, kisha kaanga na upande huo wa pili kwa muda wa dakika 2 mpaka 3, au hadi utakapo ona na upande huo wa pili umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 7.
Weka binzari nyembamba, iliki, karafuu, mdalasini, kungumanga, pamoja na basibasi, halafu koroga vizuri, halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 32 mpaka 33, au hadi utakapo ona nyama za mbavu zimeiva, kisha epua na uweke pembeni.
Washa jiko la kuoka na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto.
Chukua sufuria jingine kubwa. Weka nusu ya pilau ya binzari nyembamba uliyoipika kwenye hilo sufuria, kisha sambaza vizuri.
Weka mchanganyiko wa nyama za mbavu ulioupika juu ya hiyo pilau, kisha sambaza vizuri.
Weka nusu ya pilau iliyobaki juu ya huo mchanganyiko wa nyama za mbavu, kisha sambaza vizuri.
Chukua kikombe chenye maziwa na zafarani. Weka rosewater ndani ya hicho kikombe halafu koroga vizuri, kisha nyunyizia mchanganyiko huu juu ya pilau.
Funika vizuri sufuria hilo kwa kutumia aluminium foil. Weka sufuria hilo ndani ya jiko la kuoka, kisha oka kwa muda wa saa 1, au hadi utakapo ona biriani imeiva. Ondoa sufuria hilo kwenye jiko la kuoka na uliweke pembeni.
Nyunyizia majani ya minti kwenye hilo sufuria lenye biriani, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review